Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: TMA yaagizwa kubuni vyanzo vya mapato
Share
Notification Show More
Latest News
TBS yawataka wauza vyakula kujisajili na maeneo yao
February 3, 2023
Habari kubwa Magazetini Kenya leo February 3, 2023
February 3, 2023
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 3, 2023
February 3, 2023
Breaking: Sheikh Mkuu DSM atumbuliwa, sakata la Dr Mwaka na mkewe
February 2, 2023
Mason Greenwood afutiwa mashtaka
February 2, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > TMA yaagizwa kubuni vyanzo vya mapato
Top Stories

TMA yaagizwa kubuni vyanzo vya mapato

February 8, 2022
Share
2 Min Read
.
SHARE

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kubuni vyanzo vya mapato ambavyo ni himiilivu na visivyoumiza washitiri ili kuisaidia taasisi kujiendesha na kuendelea kutoa huduma bora na zenye viwango.

.

Naibu Katibu Mkuu Dkt. Possi amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Mamlaka hiyo na kusema kuwa ongezeko la mapato litapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya watumishi kuhama kwani mapato yataweka mazingira mazuri kwa watumishi.

.

“Nikupongeze sana Mkurugenzi Mkuu kwani kazi yako inaonekana sababu utabiri kwa sasa ni wa kuaminika kwa asilimia zaidi ya 80 lakini fikirieni kuja na vyanzo vya mapato visivyoumiza washitiri wenu ili mtumie sehemu ya mapato hayo kama motisha kwa watumishi wenu”,  amesisitiza Dkt. Possi.

Dkt. Possi amesema kuwa Serikali iko tayari kushughulikia changamoto zote zinazoikabili Mamlaka hiyo ikiwemo changamoto za kuhama kwa watumishi ili kuhakikisha taasisi hiyo inaendelea kuwa imara.

.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya hali ya hewa ili kuongeza uhakika wa taarifa kwa kuwa sekta ya hali ya hewa inazitegemeza sana sekta nyingine hususani za usafirishaji pamoja na kilimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi, amemuhakikishia Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa Mamlaka imejipanga kikamilifu kuboresha miundombinu pamoja na watumishi ili kuendeleza weledi katika sekta hiyo.

.

Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi yuko katika ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam ya kutembelea taasisi zilizo chini ya sekta hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kiutendaji na kujadili namna bora ya kupata suluhu ya chagamoto zinazowakabili.

You Might Also Like

TBS yawataka wauza vyakula kujisajili na maeneo yao

Breaking: Sheikh Mkuu DSM atumbuliwa, sakata la Dr Mwaka na mkewe

Bilioni 3.2 zatolewa kwa Wajasiriamali 16 wa Nishati safi ya kupikia

Maombi maalum Sudan Papa Francis afike salama

Gharama ya kupunguza uzito kwa puto, madhara yake?, Msechu Kilo 7 zimepungua

TAGGED: Dar es salaam, Serikali
Edwin TZA February 8, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Live:Rais Samia akishiriki kikao kazi cha wakuu wa mikoa kuhusu mfumo wa anwani za Makazi
Next Article Rais Samia awapongeza msechu na mpoto awapa majukumu ya kufanya
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

TBS yawataka wauza vyakula kujisajili na maeneo yao
Top Stories February 3, 2023
Habari kubwa Magazetini Kenya leo February 3, 2023
Magazeti February 3, 2023
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 3, 2023
Magazeti February 3, 2023
Breaking: Sheikh Mkuu DSM atumbuliwa, sakata la Dr Mwaka na mkewe
Top Stories February 2, 2023

You Might also Like

Top Stories

TBS yawataka wauza vyakula kujisajili na maeneo yao

February 3, 2023
Top Stories

Bilioni 3.2 zatolewa kwa Wajasiriamali 16 wa Nishati safi ya kupikia

February 2, 2023
Top Stories

Maombi maalum Sudan Papa Francis afike salama

February 2, 2023
Top Stories

Gharama ya kupunguza uzito kwa puto, madhara yake?, Msechu Kilo 7 zimepungua

February 2, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?