Breaking News

UPDATES: Cha kufahamu baada ya Tundu Lissu kurudishwa Polisi Central leo

on

Leo Polisi kanda maalum ya Dar es salaam walikwenda nyumbani kwa Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kufanya upekuzi baada ya Tundu kushikiliwa toka jana.

Baada ya kurudishwa kituo kikuu cha Polisi kati Dar es salaam kilichokua kinasubiriwa ni kama Tundu Lissu ataachiwa kwa dhamana ambapo mpaka jioni hii siku ikielekea kuisha CHADEMA imeeleza walipofikia.

Taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo imesema >>> “Jitihada za kuhakikisha Lissu anapata haki yake ya kisheria ya dhamana leo zimeshindikana hivyo bado yuko chini ya Polisi kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam”

“Tunasubiri utaratibu mwingine kesho wa ama kupata dhamana akiwa mikononi mwa polisi au kufikishwa Mahakamani” imeeleza taarifa ya CHADEMA

VIDEO: Matano yaliyoibuka katika kesi ya Manji Mahakamani leo…. bonyeza play hapa chini kupata taarifa kamili

JIONEE: Barabara ya magari inayopita baharini New York Marekani…. bonyeza play hapa chini kupata kila kitu

APP MPYA: Usisahau ku-install APP mpya ya ‘millardayo’ inayopatikana kwa wale wenye simu za ANDROID, kama ulikua na ile ya zamani naomba uifute…. karibu sana mtu wa nguvu, UNAWEZA KUI-INSTALL KWA KUBONYEZA HAPA >>> APP MPYA

Soma na hizi

Tupia Comments