AyoTV

VIDEO: ‘kwanini Serikali isianzishe ofisi za TRA kila Wilaya?’ -Mbunge Omari Kigua

on

Katika kipindi cha maswali na majibu bungeni leo Mei 9 2016 nakukutanisha na Mbunge wa Kilindi Omari Kigua aliyeuliza Serikali kuwa..

Ulipaji kodi ni chanzo cha mapato nchini, Serikali inao wajibu wa kuhakikisha wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi wanalipa kodi kwa mujibu wa sharia ili iweze kukusanya kodi kwa ufanisi ni lazima kuwe na ofisi za TRA katika maeneo mbalimbali

‘Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwa na Ofisi ya TRA katika Wilaya ya Kilindi?

Swali lingine likawa..’Kwa kuweka ofisi ya TRA Wilaya ya Handeni na Kuacha Wilaya ya Kilindi Serikali haioni kama inawajengwe wananchi tabia ya kukwepa kodi kutokana na umbali?

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Ashatu Kijaji amesema…’Serikali ina mpango wa kufungua ofisi za mamlaka ya mapato katika Wilaya mbalimbali nchini, uwepo wa ofisi za mamlaka ya mapato katika maendeleo yetu unaongeza ari ya wananchi kulipa kodi’

ULIKOSA HII MBUNGE KATAKA WANAOLAWITI WATOTO WAHASIWE NA SIO KIFUNGO CHA MAISHA?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments