Rais wa Togo Faure Gnassingbe amesema takriban wanajeshi 40 na raia 100 wameuawa katika vita dhidi ya magaidi kaskazini mwa Togo nchini humo.
Taifa hilo dogo la Afrika Magharibi, pamoja na mataifa jirani ya Benin, Ghana na Ivory Coast, yanazidi kukabiliwa na vitisho vya magaidi kutoka Burkina Faso na Mali.
Katika mahojiano na kituo cha kibinafsi cha New World TV Gnassingbe alisema, “Tumelipa gharama kubwa, haswa vikosi vyetu vya ulinzi na usalama, ambavyo vimepoteza karibu wanaume 40, na kisha tumepoteza raia mia moja au zaidi.”
Familia ya rais huyo imetawala Togo tangu 1967. Mahojiano hayo ya kwanza tangu achukue wadhifa wa babake mwaka 2005 yaliadhimisha miaka 63 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Ufaransa.
Aliongeza kuwa, “Kinachotokea kwetu ni aina ya hujuma makundi mawili moja linaitwa ISIS [Daesh] katika Sahara Kubwa na lingine, JNIM,” alisema, akimaanisha kundi linalohusishwa na mtandao wa kigaidi al-Qaeda.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 56, aliyechaguliwa tena mara tatu katika kura zilizopingwa na upinzani, alizungumzia wasiwasi juu uamuzi wa serikali na jeshi kubaki kimya au kutotoa taarifa mara kwa mara kuhusu mashambulizi ya kigaidi na waliouawa katika mashambulizi hayo.