Vipo vyoo vingi vya kisasa ambayo watu wengi wamekuwa wakimudu kuvitumia lakini hiki kingine kimeongezwa teknolojia zaidi kwani kina uwezo wa kufanya vitu zaidi ya tulivyozoea kutumia.
Choo hiki cha kisasa kinachoitwa Neorest ni moja ya vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya teknolojia mpya za bidhaa za elektroniki yanayoendelea huko Las Vegas.
Kina uwezo wa kujifungua unapokaribia na kujiosha, humsafisha anayekitumia kwa kifaa kinachotoa maji moto na hewa wakati mtu akiwa ameketi pia kina teknolojia inayokiwezesha kuua bakteria na virusi.
Choo hiki chenye gharama ya dola 9,800 sawa na zaidi ya milioni 20 si kwamba kitakuondolea kabisa majukumu yote ya usafi chooni, kwani hakiwezi kujiosha upande wa nje iwapo kutakuwa na uchafu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utakayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.