Duniani

Toilet Cafe? Yes.. hii ndio Moscow, kiti, bakuli vyote kwenye umbile la choo Mgahawani.. +(Video)

on

Nyumba nyingi huwezi kukutana na jiko lililo karibu kabisa na choo, kwa sababu hata matumizi ya sehemu hizo mbili yako tofauti… vipi hii ya jiko na choo kwenye chumba kimoja je?

Toilet

Kwenye vitu ambavyo vimenishtua leo na hii imo, yani watu wa Moscow Urusi wameona haja ya kuweka mambo tofauti… bango tu linalotangaza biashara limeandikwa Crazy Toilet Cafe, mgahawa ambao usishangae ukaagiza supu na ikaletwa ndani ya bakuli linalofanana na sinki la choo.. kuanzia kiti cha kukalia kina umbile hilo, mpaka mabakuli ya chakula na vyombo vingine viko hivyo !!

ToilET ii

Usishtuke mtu wangu, hapo ni kiti cha mgahawa pamoja na mto wa kuegamia,  alafu mambo mengine ya huduma yanaendelea.

Mgahawa wa aina hii ni wa kwanza kwa nchi za Ulaya, lakini unaambiwa hata Taiwan nako uko mgahawa ambao vitu vyake vya ndani vinafanana na sinki la chooni !!

Bango linasomeka hivyo nje ya mgahawa, Crazy Toilet Cafe

Bango linasomeka hivyo nje ya mgahawa, Crazy Toilet Cafe

Kila mtu anakaribishwa kwa huduma poa za msosi, na bei ni ya kawaida kabisa kwa hiyo sio mahali pa kupaogopa… mfano ukafunguliwa mgahawa wa hivi Bongo utatamani kwenda na mtu wako mkaenjoy lunch?

Toi II

Hii hapa video ya Mgahawa wa Crazy Toilet Cafe uliofunguliwa Moscow, Russia..

Kama hukuwahi kuijua ya mgahawa wa hivyo Taiwan nayo hii hapa mtu wangu

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments