Michezo

Toni Leinstner aomba radhi kwa kumvaa shabiki

on

Beki wa Humburg SV ya Ujerumani Toni Leistner ,30, ameomba radhi kwa kitendo chake cha kutoka uwanjani na kwenda kumvaa shabiki wa Dynamo Dresden aliyemkwaza.

Toni alienda jukwaani katika mchezo ambao Humburg walipoteza 4-1 mchezo wa Kombe la DFB-Pokal na kumsukuma shabiki yule aliyekuwa kamtolea maneno ambayo hakuyapenda.

Walinzi (Steward) wa uwanja hapo walimuwahi na kuamua ugomvi huo kwa kumtuliza Toni na kuondoka katika jukwa alilokiwa amekaa shabiki huyo.

Soma na hizi

Tupia Comments