Michezo

TOP 5 Stories: Huyu ndio mrithi wa Mourinho Chelsea, Man United na Lewandowski? Man City na mipango ya Guardiola..

on

Kabla siku haijaisha mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee stori 5 za soka zilizoingia katika headlines siku ya December 17, kuna mengi yamezungumzwa katika stori za soka December 17 ikiwemo stori za kufukuzwa kwa mara ya pili kwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho. Hizi ndio TOP 5 ya stori za soka December 17.

5- Chelsea kumtoa kwa mkopo Djilobodji katika klabu ya Marseille

Klabu ya soka ya Chelsea inajiandaa kumtoa kwa mkopo Papy Djilobodji kwenda katika klabu ya Olympique Marseille, uhamisho ambao watafanya katika dirisha dogo la usajili la mwezi January.

Djilobodji

4- Chelsea kumsajili Pele

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho anatajwa kuwa alikuwa kamjumuisha katika mipango ya Chelsea mshambuliaji wa klabu ya Southampton Graziano Pelle ili kutatua tatizo la ushambuliaji ambalo linaikumba klabu hiyo kwa sasa.

Football - Chelsea v Southampton - Barclays Premier League - Stamford Bridge - 3/10/15 Graziano Pelle celebrates after scoring the third goal for Southampton Reuters / Dylan Martinez Livepic EDITORIAL USE ONLY. No use with unauthorized audio, video, data, fixture lists, club/league logos or "live" services. Online in-match use limited to 45 images, no video emulation. No use in betting, games or single club/league/player publications. Please contact your account representative for further details.

3- Man City wanajiandaa kutoa ofa kubwa kwa Pep Guardiola

Inaripotiwa kuwa klabu ya Man City ipo tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha ili kumpata kocha chaguo lao namba moja Pep Guardiola. Man City inatajwa kumpa mshahara wa pound milioni 15 kwa mwaka.

Pep-Guardiola6

2- Klabu ya Chelsea inatajwa kumleta Hiddink ili awe mrithi wa Mourinho

Klabu ya Chelsea inatajwa kumleta kocha wa kirusi aliyewahi kuifundisha klabu hiyo Guus Hiddink ili arithi mikoba ya Jose Mourinho ambaye anatajwa kutofikia malengo ya klabu kwa msimu huu.

Jose-Mourinho110

1- Man United wanamtaka Lewandowski

Man United inatajwa ipo tayari kuwapiku PSG katika mbio za kumsajili mshambuliaji mahiri wa klabu ya FC Bayern Munich Robert Lewandowski . Licha ya kuwa Man United wamemuahidi mshahara wa pound milioni 15 kwa mwaka kama PSG, ila wanatajwa kuongeza nguvu za kumpata.

Lewandowski5

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments