Duniani

List ya nchi 5 zilizotumia fedha nyingi kwa ajili ya majeshi 2016

on

Inaelezwa kuwa sifa ya nchi yoyote ni uwezo wa Jeshi lake katika kujilinda na kupambana kwa ajili ya wananchi ambapo tumekuwa tukishuhudia gharama inayotumika kuhakikisha Idara hiyo inaimarika kwa kulipa mishahara minono na kununua vifaa vya kisasa.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm ‘SIPRI’ zimetajwa nchi 5 zinazotumia fedha nyingi zaidi kwa ajili ya Jeshi hadi kufikia 2016 zikiongozwa na Marekani.

SIPRI imesema kuwa matumizi ya dunia katika majeshi yaliongezeka hadi Dollar 1.7 trillion mwaka 2016 ambapo Marekani inasalia kinara kwa kutumia fedha nyingi kwenye jeshi mwaka 2016 ambapo matumizi yameongezeka kwa 1.7% kuifanya ifikishe Dollar 611 billion.

China ilitumia Dollar 215 billion na kuifanya kukamata katika nafasi ya pili huku Urusi ikikamata nafasi ya tatu ikitumia Dollar 69.2 billion. Saudi Arabia inakamata nafasi ya nne ikitumia Dollar 63.7 billion na India katika nafasi ya tano ikitumia Dollar 55.9 billion.

VIDEO: Makomando wa JWTZ wakionyesha uwezo mbele ya JPM. Bonyeza play kutazama…

Soma na hizi

Tupia Comments