Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya October 5, 2016 ni hii kutoka gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Kukaa muda mrefu husababisha Saratani’
#MTANZANIA UTAFITI: Watu wanaokaa sehemu moja kwa zaidi ya saa nne wanakabiliwa na magonjwa ya kisukari, moyo, shinikizo la damu, saratani pic.twitter.com/ONR0rDSRO9
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
Imeelezwa kuwa watu wanaokaa kitako maofisini au kwenye foleni za magari kwa zaidi ya masaa manne wako katika hatari ya kupata magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza ikiwemo magonjwa ya Moyo, Shinikizo la Damu, Saratani na Kisukari.
Kwa mujibu wa Dr. Fredrick Mashili kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) amesema sababu kubwa inayopelekea watu kupata magonjwa hayo ni kukaa muda mrefu maofisini au kwenye foleni na kutofanya mazoezi baada ya kutoka makazini.
Akitolea mfano wa ripoti ya hivi karibuni kutoka Shirika la Moyo la Marekani lilichapisha makala yenye kichwa cha habari “International Cardiovascular Desease Statistics” limeeleza kuwa kutofanya mazoezi na kula vyakula visivyofaa ni moja ya mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa magonjwa hayo.
Dr. Mashili ameeongeza kuwa kukua kwa Teknolojia kumechangia watoto kukosa muda wa kucheza badala yake hupendelea kukaa na kucheza michezo ya kwenye kompyuta na video (Gaming), tatizo ambalo ni kubwa kwao kwasababu hupelekea watoto kutojiheshimu, kuwa na wasiwasi mwingi na kufadhaika kila wakati.
#NIPASHE Rais Magufuli ameeleza kuwa kwenye bandari ya Dar es salaam baadhi ya mabosi walikuwa wakibeba fedha kwenye buti ya gari pic.twitter.com/ddIoOD9zuE
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#NIPASHE Wauzaji wa mitungi ya gesi za majumbani watakiwa kuwa na mizani ktk vituo vyao vya kuuzia noshati hiyo ili wateja wahakikishe ujazo pic.twitter.com/WEdrvGdAky
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#NIPASHE Baada ya kuzihoji wizara, taasisi 8 PPRA imezikabidhi TAKUKURU kutokana na kubaini kuwapo kwa rushwa ktk utoaji wa tenda, manunuzi pic.twitter.com/ghbMa9FLPy
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#NIPASHE JPM aagiza wakimbizi kutoka DRC waliopo TZ kurudishwa baada ya Rais Kabila kumhakikishia kuwa hali ya usalama nchini mwake ni nzuri pic.twitter.com/6sBs4Q6US7
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#NIPASHE TFDA imetangaza vita dhidi ya wanaotangaza ktk mitandao ya kijamii biashara ya vipodozi hatarishi vilivyopigwa marufuku nchini pic.twitter.com/uLQ9C9WOjk
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#NIPASHE Mke wa Waziri ambaye alikuwa akifanya kazi ATCL adaiwa kuandika barua ya kuacha kazi, ni siku chache tangu JPM ahoji kuwapo kwake pic.twitter.com/v0kcRALkQV
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#MWANANCHI Bodi ya wadhamini CUF yaunga mkono msimamo wa msajili na kupanga kuwakutanisha Prof. Lipumba na Maalim Seif ili kumaliza mgogoro pic.twitter.com/4ZHURbO9UJ
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#MWANANCHI Wizara ya afya imesema chanjo zilizoadimika nchini, zimewasili na wananchi watapata huduma kuanzia sasa pic.twitter.com/s3NJIfAHRE
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#MWANANCHI Watu 21wamefariki dunia kwa ugonjwa usiofahamika ktk kata ya Pinyinyi, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha pic.twitter.com/W8ziKxQTVi
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#MWANANCHI Rais Magufuli safari 2, Rais Mstaafu Kikwete safari 25, ni tathmini ya safari ambazo kila mmoja amefanya ktk miezi 11 ya kwanza pic.twitter.com/RyyrwQeM1L
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#MAJIRA Ewura watangaza bei mpya za kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli ambazo zimepungua ikilinganishwa na zile za mwezi uliopita pic.twitter.com/eMXsFlntuX
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#MAJIRA Takwimu za wagonjwa wa afya ya akili nchini zinaonesha kati ya watu wazima wanne mmoja wao anakabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo pic.twitter.com/QPWASzDftJ
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
#MTANZANIA Wanakijiji Mvumi Dodoma waliwaua watafiti baada ya kuwahusisha na mfanyabiashara ambaye amekuwa akihusishwa na vifo kijijini hapo pic.twitter.com/dvXaSrx6oU
— millardayo (@millardayo) October 5, 2016
ULIPITWA NA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV? TAZAMA HAPA CHINI