Michezo

Baada ya ushindi wa mechi zaidi ya 6 mfululizo, April 17 Simba imepokea kipigo dhidi ya Toto Africans

on

Baada ya klabu ya Simba kukaa kileleni kwa muda kwa kuwazidi michezo watani zao wa jadi Dar es Salaam Young Africans, April 16 Yanga walirejea kileleni baada ya kumaliza michezo yao ya viporo, lakini Simba walikuwa wanapewa nafasi ya kurudi tena kileleni leo April 17 2016 kama wangeshinda mchezo wao dhidi ya Toto Africans.

Kwa bahati mbaya leo April 17 uwanja wa Taifa Dar es Salaam Simba wamekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Toto Africans na kuendeleza rekodi yao ya kusumbuliwa na Toto kila mara wanapokutana. Simba kabla ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu walikuwa na rekodi ya kushinda mechi zaidi ya 6 mfululizo baada ya kufungwa na Yanga mzunguuko wa pili.

DSC_0476

Toto Africans waliifunga Simba dakika ya 21 kupitia kwa kupitia kwa mshambuliaji wao Waziri Junior ambaye alitumia umahiri mkubwa wa kupokea mpira na kuuweka kifuani halafu kupiga shuti nje ya 18 na kumshinda golikipa wa Simba Vicent Agban.

kipigooooo

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania leo April 17 2016

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

KAMA ULIKOSA VIDEO YA MAGOLI YA MECHI YA SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016

Soma na hizi

Tupia Comments