Michezo

Tottenham wababe wa Chelsea, Lamela apindua matokeo

on

Usiku wa Septemba 29 2020 ulichezwa mchezo wa round ya nne wa michuano ya Kombe la Carabao kwa kuzikutanisha timu za London Tottenham dhidi ya wageni wao Chelsea.

Mchezo huo ulianza kwa Chelsea kupata goli la kuongoza dakika ya 19 kupitia Werner goli ambalo lilidumu na kila mtu kuanza kuamini kuwa kutokana na mchezo kufikia hadi dakika ya 80 Chelsea akiongoza 1-0 basi Chelsea kamashamaliza.

Kumbe haikuwa hivyo jitihada za Lamela dakika ya 84 zikazaa matunda na kuisawazishia goli Tottenham dakika ya 84 na kufanya dakika 90 zimalizike kwa kufungana magoli 1-1.

Mchezo huo baada ya hapo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati na Tottenham kusonga mbele kwa kushinda penati zote 5 na Chelsea kushinda penati 4 huku penati yao ya tano Mason Mount akikosa na kuifanya Chelsea iage michuano hiyo.

Soma na hizi

Tupia Comments