Stori za kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast anayekipiga katika klabu ya Manchester City Yaya Toure kutokuwa na raha klabu hapo zimekuwa zikiingia katika headlines mara kwa mara, awali kulikuwa na stori za kiungo huyo kutaka kuhama Man City kutokana na kutokuwa na furaha klabuni hapo.
Toure ambaye wiki kadhaa nyuma aliongea na gazeti la kifaransa na kueleza kuwa hana furaha moja kati ya vitu vinavyomnyima furaha ni waandishi kujadili mshahara wake, hivyo hata katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August alikuwa anatajwa kukaribia kuhama klabu hiyo.
October 28 katika kitabu cha ‘Pellegrini’s Methods’ Yaya Toure ametaja mtu pekee aliyesababisha yeye kuendelea kubakia Man City ni kocha wa klabu hiyo Manuel Pellegrini, ambaye amekuwa kama baba kwake katika kila kitu alichokuwa anafanya. Manuel Pellegrini anatajwa kuwa karibu na kiungo huyo hata kuna wakati alimtetea kuwa uwezo ulishuka baada ya kuwa na mawazo ya kufiwa na mdogo wake Ibrahim Toure.
“Nilibaki kwa sababu ya Manuel siku zote amekuwa akiongea na mimi na kunipa ushauri, amekuwa ni mtu wa karibu na maisha yangu ya nje ya uwanja, amekuwa kama baba kwangu nikiwa katika wakati mgumu sikuwahi kujisikia hivyo kwa kocha mwingine yoyote”>>> Yaya Toure
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.