Mix

VIDEO: Mipango ya TPDC kusambaza gesi asilia DSM na Pwani

on

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ‘TPDC’ limeelezea kuhusu miradi mbalimbali ya usambazaji wa nishati ya gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na mikoa mingime ya Tanzania.

TPDC imesema kwa mwaka huu 2017, wamepanga kufanya upembuzi yakinifu wa mradi wa uendeshaji wa ujenzi wa mtandao wa mabomba ya kusambaza gesi asilia ndani ya jiji la Dar es Salaam ambapo Mshauri Mwelekezi wa kazi hiyo anatarajiwa kupatikana June 2017.

Ayo TV na millardayo.com imekutana na Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Kapuulya Musomba ambaye ameelezea na kuweka wazi mipango ya Shirika hilo.

“Kuna bomba la zaidi ya Kilometa 500 kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam na litaendelea kuongezeka. Kwa bomba hilo kuwepo, maana yake ni kwamba, mahali popote katika Kilometa 500, unaweza ukaweka kiwanda ukapata nishati kwa ajili ya umeme.” – Kapuulya Musomba.

Bonyeza play kwenye video hapa chini…

VIDEO: Hatua iliyofikiwa na Dangote Cement na TPDC kuhusu gesi asilia. Bonyeza play kutazama.

Soma na hizi

Tupia Comments