Michezo

Mafanikio ya Pep Guardiola hayamshitui Eto’o bora kwake Mourinho

on

Staa wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na club ya FC Barcelona ya Hispania Samuel Eto’o ameeleza mawazo yake kufuatia swali alilouliza kuhusiana na uwezo wa makocha wawili kati yakocha Jose Mourinho na Pep Guardiola wa Man City ni yupi bora kwa sasa kwa upande wake.

Katika mahojiano na The Sun Eto’o amemtaja Jose Mourinho kuwa ndio bora kwake kutokana na mafanikio yake, licha ya kuwa Pep Guardiola ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza England kutwaa mataji yote matatu ya ndani, Eto’o ana mkubali Mourinho kwa kutwaa Champions League akiwa na Porto 2004 na Inter Milan 2010.

Eto’o kamtaja Mourinho kwa sababu ametwaa UEFA Champions League akiwa na vilabu viwili tofauti wakati Pep Guardiola ameweza kutwaa Champions League mara mbili pia (2009-2011) akiwa na FC Barcelona pekee na FC Bayern alifeli.

“Siwezi kumlinganisha Jose Mourinho na Pep Guardiola kwa sababu mmoja ameshindwa kutwaa Champions League akiwa na FC Bayern Munich wakati mwingine amewahi kufanya hivyo akiwa na FC Porto hilo liko wazi”>>> Samuel Eto’o

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments