AyoTV

VIDEO: Niyonzima kaeleza kilichotokea kati yake na Simba SC

on

Kiungo wa zamani wa Simba SC Haruna Niyonzima kwa sasa amerejea nyumbani kwao Rwanda na kujiunga na club ya AS Kigali ya nchini humo, Niyonzima licha ya kuonesha uwezo wa juu msimu uliopita kiasi cha wengi kutarajia kuwa atapewa mkataba mpya Simba SC, ameondoka kwao na kuwaacha wengi wakijiuliza ni nini kilitokea.

Haruna leo alikuwa uwanja wa Taifa na timu yake ya AS Kigali kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kuwania kucheza hatua ya Makundi ya michuano ya Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya KMC, pamoja na kuwa hakucheza mchezo huo walioshinda 2-1 na kuitoa KMC, Niyonzima kaweka wazi nini kilitokea akaondoka Simba SC.

“Mimi siwezi kulizungumzia sana hilo lakini niseme tu kwamba nilikuwa nimemaliza mkataba wangu, mwisho wa siku timu inapomaliza mkataba kama imeongea na wewe au haijaongea na wewe, sioni kama ni kikubwa lakini nilikuwa na mipango ya kurudi nyumbani (Rwanda) kwa sababu ya familia yangu unajua nimekaa sana mbali na familia yangu”>>>>Niyonzima

VIDEO: Kwa tathmini hii ya Edo Kumwembe, Mashabiki wa Chelsea haina budi kuwa wavumilivu

Soma na hizi

Tupia Comments