Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Yusuph Mwenda amesema Zanzibar na Bara hakupaswi kua na changamoto za Kodi akigusia changamoto zinazojitokeza pindi wasafiri watokao Zanzibar ama Bara kutozwa kodi kwa bidha ndogo ndogo
Mwenda ameahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazojitokeza na kufikia wakati itakua ni rahisi kufanya biashara kati ya Zanzibar na Tanzania Bara ,huku akikiri kuwepo kwa changamoto hizo na kwamba mifumo ya Zra na Tra sasa inaowana na ifikapo mwezi wa sita changamoto hizo kwisha
Mwenda ameyasema hayo Zanzibar kwenye Ghafla iliohudhuriwa na Makamo wa kwanza wa Rais Hemed Suleiman Abdullah wakati akiwakabidhi tuzo walipakodi Bora na waliofanya vizuri kwenye kulipa kodi.