Katika kuhitimisha kilele cha siku ya mlipakodi mamlaka ya mapato TRA mkoa wa iringa wametembelea vituo vya kulelea watoto yatima kituo cha Tosamaganga na kituo cha Amani kilichopo kata ya kitwiru.
Akizungumza wakati wa matukio hayo mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani TRA Ally Mnyani ambae alimuwakilisha kamishna mkuu wa TRA Yusuph Mwenda amesema wao kama TRA wana utaratibu wa kurudisha fadhila kwa wadau mbalimbali wa kodi ikiwa ni pamoja na kutembelea watu wenye uhitaji kwani na wao ni wadau wa kodi.
Mnyani amewapongeza viongozi wa vituo vyote viwili kwa malezi na maadili wanayowapa watoto hao kwani bila malezi kutoka kwa viongozi ingeweza kupelekea watoto hao kuwa watu wabaya.
Tunategemea kwa malezi mnayowapa hawa watoto tutapata walipakodi wazuri hapo baadae, Alisema Mnyani.
Aidha meneja wa TRA mkoa wa Iringa John Jackson Eliona amesema vitu vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 5.3 vimetolewa kwa vituo vyote viwili ili kuwarudishia tabasamu kwa watoto hao.
Jackson amesema walipakodi wa mkoa wa Iringa wamefanya vizuri sana na kuvuka lengo ambapo Zaidi ya bilioni 30 zimekusanywa kwa mkoa wa Iringa hivyo hawana budi kupongezwa.
Kwa upande wao wasimamizi wa vituo hivyo Bi Elizabeth Mwakabanga na Sister Joyce Mtatifikolo wameushukuru uongozi wa TRA mkoa wa Iringa kwa kuwafikia na kuwapa msaada huo huku wakisisitiza kwa siku nyingine kutembelewa hata tu kwa kuwapa faraja watoto hao n alo ni jambo kubwa