Mamlaka ya Mapato Tanzania Tra Mkoa wa Iringa Imeendelea kudumisha mahusiano Mazuri na kuwashukuru wafanyabiashara wake Mkoani hapa kwa kuendelea kutimiza wajibu wao wa kulipa Kodi kwa wakati
Shukrani hizo zinetolewa leo baada ya Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania Tra Mkoa wa Iringa Bw. Peter Jackson akiwa pia ameambatana na meneja msaidizi Bw. Gwamaka Pholld walipowatembelea walipakodi Mbalimbali eneo la Miyomboni kwa ajili ya kuwashukuru kwa kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi lakini pia kusikiliza changamoto mbalimbali za kikodi na kuzitatua
Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa amesema ni muhimu kutimiza wajibu wa kulipa kodi kwa wakati ili kuondokana na adhabu zitokanazo na kuchelewa kulipa kodi.
Pia amesisitiza matumizi sahihi ya Mashine za kutolea Risiti za Kielektroniki yaani wauzaji wanapaswa kutoa risiti za Kielektroniki kila wanapofanya Mauzo, na wanunuzi kudai risiti kila wanapofanya Manunuzi.