Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Geita imetoa Semina kwa wafanyabiashara wakubwa wanaofanya shughuli mbalimbali ikiwemo hoteli pamoja na nyumba za kulala wageni mkoani humo.
Akizungumza mara baada ya Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Geita (GEDECO) Ndg.Justine Katiti Afisa Huduma Mlipa kodi TRA mkoa wa Geita amesema lengo la semina hiyo ni kutoa maelekezo juu ya wajibu wao wanaotakiwa kuufata katika kukusanya tozo ya kulala usiku (Bed Night leavy) kama ambavyo Mabadiliko yanavyowaelekeza.
“Changamoto mahudhurio siyo mazuri make hapa Geita Mjini tuna hoteli ambazo zimeainishwa kukusanya Bed Night Leavy ni zaidi ya 90 kwa hiyo wamekuja watu kama nusu au sitini lakini vilevile wanaokuja unakuta sio wale walipa kodi wenyewe ko wanatuma watu ambao ni wasaidizi wao, “ Afisa Huduma Mlipa Kodi Geita.
Katiti amesema changamoto kubwa ambayo wamekuwa wakikumbana nayo ni pamoja na Mahudhurio kutokuwa mazuri katika semina ambazo wamekuwa wakiwaita wateja wao kwa ajili ya kutoa semina, elimu na maelekezo mbalimbali yanayomfaa mteja wao huku akiwaomba wamiliki wa nyumba hizo za kulala wageni pamoja na wamiliki wa hoteli kuhakikisha wanahudhuria wao wenyewe na si kutuma wawakilishi.
Kwa upande wake Afisa Viwanda Biashara na uwekezaji Halmashauri ya Mji wa Geita Suleiman Said Muharanga amesema semina hiyo ina lengo la kukusanya kodi ya usiku ambayo Serikali kupitia TRA inatoa maelekezo kwa wateja wake kuhakikisha wanakusanya kodi hizo kama sheria inavyowataka .
John Christian na Michael Shuka ni Meneja kutoka Nyumba mbalimbali za kulala wageni Mkoani Geita wameiomba serikali kuondoa tozo hiyo ya Bed Night leavy kwani inaleta Mkanganyiko kwa maana ina hizo nyingine ambazo ni asilimia 18 ya VAT kutoka TRA.