Habari za Mastaa

Mchekeshaji Tracy Morgan katika hali mbaya baada ya ajali.

on

tracyMchekeshaji maarufu wa nchini Marekani Tracy Morgan bado yupo katika hali mbaya kiafya kutokana na ajali mbaya ya gari aliyopata mwishoni mwa wiki.

Muigizaji huyo wa vichekesho anakabiliwa na majeraha ya kuvunjika mbavu, pua na mguu baada ya gari aliyokuwa akisafiria kugongwa na gari kubwa na kusababisha ajali mbaya.

tracy2Baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake, Morgan ameanza kuonyesha matumaini lakini ataendelea kubaki hospitalini kwa wiki kadhaa akipatiwa matibabu, kwa mujibu wa msemaji wake.

Katika ajali hiyo iliyotokea mjini New Jersey muigizaji mwingine wa vichekesho Jimmy Mack, alipoteza maisha.

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.

 

Tupia Comments