Maduka ya wafanyabiashara zaidi ya kumi na nyumba za kulala wageni pamoja biashara mbalimbali zinadaiwa kufungwa kutoka kwa kukosekana kwa umeme kwa zaidi ya siku 4 huku chanzo kikidaiwa ni kupasuka na kuungua kwa trasifoma iliyopo katika stand ya kikatiti kata ya kikatiti wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha
Wananchi pamoja na wafanyabiashara hao wakizungumza na waandishi wa habari pembezoni mwa trasfoma hiyo wamesema kwamba kukosekana kwa umeme katika eneo hilo imeathiri zaidi ya wananchi elfu moja huku wengine wakishindwa kuendesha biashara zao na kupata hasara licha ya kutoa taarifa kwa mamalaka husika na kutofanyiwa kazi.
Akizungumzia changamoto hiyo meneja wa shirika la umeme tanesco wilaya ya Arumeru Mhandisi Mathew Sichilima amesema tayari wameshafika eneo hilo na wameanza kuwahamishia wananchi kwenye transfoma za jirani ili wapate umeme wakati wakishughulikia tatizo hilo la transomer kuungua