Habari za Mastaa

Trevor Noah kwenye headlines, azindua rasmi show ya The Daily Show Marekani akiwa na staa huyu..!

on

Mchekeshaji kutoka South Africa, Trevor Noah aliweka headlines nyingi sana Africa pamoja na dunia nzima baada ya kuchaguliwa kuwa mtangazaji mpya wa kipindi cha comedy kiitwacho The Daily Show nchini Marekani, kipindi kinachoruka kupitia channel ya Comedy Central huko huko Marekani.

NOAH3

Trevor Noah na Actor Jamie Foxx.

Good news mtu wangu, jana tarehe 28 September Trevor Noah aliruka LIVE kwa mara ya kwanza kwenye The Daily Show na bila kupoteza muda staa huyo kutoka South Africa alianza na kuwavunja watu mbavu kwa vichekesho vyake vikali… licha ya hayo kwenye uzinduzi wa episode yake ya kwanza jana, Trevor alisindikizwa na staa mkubwa wa comedy Marekani Kevin Hart!

NOAH

Staa wa comedy Marekani, Kevin Hart akiwa na Trevor Noah kwenye kipindi cha The Daily Show siku ya jana!

Trevor Noah ambaye amekuwa mtu wakumuangalia sasa hivi alipost picha siku chache zilizopita kwenye page yake ya Instagram kutoa ratiba ya mastaa wote watakaomsindikiza wiki hii mzima… jana ilikuwa mchekeshaji Kevin Hart, leo itakuwa zamu ya Whitney Wolfe Mkurugenzi wa kampuni ya Bumble Marekani, jumatano Trevor Noah atasindikizwa na Gavana wa New Jersey Chris Chrisite na Alhamisi mwanamziki Ryan Adams ataungana na Trevor kwenye kipindi chake cha The Daily Show!

NOAH2

Ratiba ya wageni watakaoonekana kwenye kipindi cha The Daily Show wiki hii.

 

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments