Top Stories

Cha kufahamu kutoka Shirika la Reli Tanzania

on

Shirika la Reli Tanzania TRL leo September 15, 2017 limeeleza mabadiliko machache ya ratiba ya treni ya abiria kwa safari za kati wiki ijayo kutokana na marekebisho na maboresho katika daraja la Kilometa 209/8 kati ya Morogoro na Mazimu.

Treni ya Jumanne September 19 ya kwenda bara haitakuwepo pamoja na treni ya Alhamis September 21 ya kutoka bara ambapo treni hizi ni zile zinazopita Shinyanga, Tabora, Dodoma kuja Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa May 15 mwaka huu wakati wa mvua kubwa kulitokea ajali eneo hilo na na hivyo shirika lilifanya marekebisho ya dharura na kwahiyo wahandisi wa kampuni hiyo wameona huu ni wakati muafaka wa kufanya marekebisho eneo hilo kwa ajili ya usalama wa safari za treni.

Uliiona hii? MWANZO MWISHO! RC Mwanza alivyoamua kufanya kazi usiku nje ya ofisi

Hii je?RC MWANZA! Kaacha ofisi kuwafuata Wananchi, unamweleza changamoto zako

Soma na hizi

Tupia Comments