Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema tayari Serikali imetenga kiasi cha fedha shilingi Tirioni 1.3 kwa Mwaka wa Fedha ambacho kimetumika kuwapandisha madaraja watumishi zaidi ya laki 6 kutoka kada mbalimbali ikiwemo Kada ya uwalimu.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na Walimu wilayani Bukombe Mkoani Geita katika kuadhimisha siku ya walimu wilayani Bukombe ambapo amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 229.9 zimetumika kulipa Malimbikizo ya watumishi zaidi ya laki moja na 43 ikiwemo Kada ya uwalimu na kuwataka Wakurugenzi katika Halmashauri , Maafisa elimu kuweka Mifumo ya kusikiliza walimu (Vijijini).
Majaliwa amesema Serikali imeendelea kubadilisha watumishi kutoka kada mbalimbali ambapo zaidi ya watumishi Elfu 36 wamebadilishwa kada na kiasi cha shilingi Bilioni 3 kimetumika .
Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt.Doto Mashaka Biteko amewataka walimu kote nchini kuendelea kuwa na Moyo wa kuwaandaa watoto katika malezi yaliyo bora huku akiwapongeza walimu wote kwa kuendelea kuwa Moyo wa Huruma na Malezi mema kwa wanafunzi.
Mkuu wa Mkoa wa Geita , Martine Shigela amesema zaidi ya watumishi 15000 katika mkoa wa Geita tayari wamekwisha kupandishwa Madaraja ikiwemo Kada ya Uwalimu ambapo watumishi 940 wamebadilishiwa kada huku akiipongeza Serikali ya awamu ya Sita kwa kuendelea na kujali Sekta ya Elimu (Walimu).