Usiku wa July 26 2016 eneo la Kariakoo Kamata Dar es Salaam iliripotiwa kutokea ajali ya basi la UDA lenye namba za usajili T 696 CVP linalofanya safari zake kati ya Mbagala na Kariakoo liligongana na treni, taarifa za awali zinataja kuwa watu zaidi ya 40 wamejeruhiwa na mmoja kupoteza maisha.
Leo July 29 2016 Afisa habari wa kampuni ya reli Tanzania ‘TRL’, Midraj Maez ameizungumzia ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la abiria kuvunja sheria na kukatiza barabara ya treni ikiwa magari yote yamesimamishwa kupisha kichwa cha treni kupita. Dereva wa basi hilo alivunjika miguu na yupo katika uangalizi wa vyombo vya dola kwa hatua za kisheria zaidi.
ULIKOSA HII AJALI YA TRENI NA BASI LA UDA JULY 26 2016 DAR ES SALAAM? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI