Kuna ajali ambazo humfika binadamu katika mazingira mbalimbali ambazo husababisha vifo na wakati mwingine ulemavu wa kudumu, sasa wenzetu majuu wamekuwa katika juhudi mbalimbali kuwafanya watu wa namna hiyo kuendelea na maisha yao.
Leo April 10, 2017 nimekutana na stori hii ambayo unaambiwa mtu amekatika viganja vyote viwili lakini amewekewa viganja vya mtu mwingine na anaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Habari hiyo iliripotiwa na mtandao maarufu wa Daily Mail April 06, 2017, inamtaja Chris King, 57, ambaye alipoteza viganja vyote – isipokuwa vidole gumba pekee – kwenye ajali iliyotokea miaka minne iliyopita akiwa kazini.
Baada ya kufanyiwa operation July na wataalam wa Leeds General Infirmary (LGI) kuwekewa viganja hivyo, alianza kufanya mazoezi na sasa anaonekana kuendelea vizuri akiandika na kujitengenezea chai.
AJALI YA TRENI TANZANIA: Ilitokea Ruvu Pwani. Bonyeza play kutazama.