Top Stories

Trump aitishia India kisa Chloroquine

on

Rais Trump ametishia kulipiza kisasi dhidi ya India endapo Nchi hiyo itapiga marufuku mauzo ya dawa ya Hydoxy-chloroquine, Trump amedai dawa hiyo inaweza kutibu Corona, India ambayo ni mzalishaji mkuu wa dawa hiyo Duniani imepiga marufuku dawa hiyo kuuzwa nje.

Rais Trump amesema amezungumza na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na kumwambia kuwa Marekani inataka izipate dawa za Hydroxy-chloroquine ilizoagiza kutoka India ili zisaidie kuwatibu wagonjwa corona na kusema kitendo cha India kupiga marufuku dawa hizo kuuzwa nje hakikubaliki.

Dawa hiyo inatumika kutibu wagonjwa wa Malaria lakini sasa Trump amekuwa akiinadi na kuwa inatibu corona ambapo tayari sasa hivi inafanyiwa majaribio kubainisha iwapo inaweza kutumika kutibu kwa uhakika ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na maambukizi wa virusi vya corona.

CORONA: MAGARI YALIYOKOSA SANITIZER YAKAMATWA “HATUFANYI MASIHARA NA CORONA”

Soma na hizi

Tupia Comments