Donald Trump, mgombea wa Urais kutoka Chama cha Republican, ametangaza mpango wa kuunda tume ya ufanisi wa Serikali ambayo itakuwa chini ya uongozi wa bilionea Elon Musk, ikiwa atashinda uchaguzi wa Novemba 5.
Akizungumza katika Klabu ya Uchumi ya New York, Trump pia aliahidi kupunguza viwango vya kodi kwa kampuni zinazozalisha bidhaa nchini, kuanzisha maeneo yenye kodi ndogo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya, na kuanzisha mfuko wa taifa.
Trump alisema kuwa Tume hiyo itafanya ukaguzi wa kifedha na utendaji wa Serikali kuu na itapanga mikakati ya kuondoa udanganyifu na malipo yasiyo sahihi ndani ya miezi sita.
Aidha Musk alikiri mazungumzo na Trump kuhusu Tume hiyo na kusema atafurahi kujiunga na Tume hiyo bila malipo yoyote.
Mpango huu umepokelewa kwa maoni mchanganyiko, baadhi wakipinga kwa kusema unalenga kupunguza idadi ya wafanyakazi wa Serikali, wakati wengine wakiona kama hatua ya kuboresha Ufanisi wa Serikali.
SOURCE