Top Stories

Trump amuokoa Lil Wayne kifungo cha miaka 10

on

Rais Trump amewasamehe Watu zaidi ya 70 wenye makosa mbalimbali muda mfupi kabla ya kuondoka Ikulu ambapo miongoni mwa waliosamehewa ni Rapper Lil Wayne ambae alikua na hatia ya kumiliki silaha kinyume na sheria ambapo msamaha huu unamfanya anusurike na kifungo cha hadi miaka 10 Jela katika hukumu ambayo ingetolewa January 28 2021.

Lil Wayne amekua upande wa Donald Trump kitambo na hata kwenye kampeni zake amekua akionesha waziwazi kum-support Trump kitendo ambacho kilifanya akosolewe sana na Watu wengi Marekani.

Rapper mwingine aliepata mabadiliko ya msamaha wa Rais Trump ni Kodak Black ambae wakati msamaha huu wa Rais unatoka bado alikua gerezani ambae pia alikamatwa kwa makosa ya silaha.

RAIS MAGUFULI AKIMKAMUA NG’OMBE MAZIWA

Soma na hizi

Tupia Comments