Donald Trump amesema anapanga kujisalimisha siku ya Alhamisi katika mahakama ya jimbo la Georgia kujibu mashtaka ya kuingilia uchaguzi.
Jaji mmoja mjini Atlanta ambaye anasimamia kesi ya rais huyo wa zamani ameweka dhamana ya $200,000 (£157,000).
Makubaliano hayo yanasema Bw Trump anaweza kubaki huru akisubiri kesi yake ilimradi asijaribu kutishia au kuwatisha mashahidi.
Bw Trump anakanusha mashtaka 13, yakiwemo ya ulaghai na taarifa za uongo.
‘Mshtakiwa hatafanya kitendo chochote cha kumtisha mtu yeyote anayejulikana kuwa mshtakiwa mwenza au shahidi katika kesi hii au kuzuia utendakazi wa haki vinginevyo’ilisema jalada la mahakama lililotumwa Jumatatu.
Baadaye siku ya Jumatatu Bw Trump alichapisha kwenye mtandao wake wa kijamii,Truth Social: ‘ unaweza kuamini? Nitaenda Atlanta, Georgia, Alhamisi’