Top Stories

Trump aondolewa ghafla kwenye mkutano na maafisa usalama wake ‘secret service’

on

Rais wa Marekani Donald Trump, Jumatatu jioni ghafla aliondolewa na maafisa wanaolinda usalama wake, kutoka kwenye chumba alichokuwa akiwahutubia waandishi wa habari ndani ya Ikulu mjini Washington, kufuatia kisa cha mtu kupigwa risasi karibu na Ikulu hiyo.

Trump alikuwa tu ameanza kusoma hotuba yake wakati afisa mmoja wa idara ya Secret Service, alipomkaribia na kumnong’onezea na kiongozi huyo akaondoka kwenye jukwaa na kuwaacha waandishi wa habari chumbani humo bila kusema chochote.

Kulikuwa na hali ya wasiwasi huku wanahabari wakijaribu kufahamu ni nini kilikuwa kimetokea.

Dakika chache baadaye, Rais huyo alirejea na kuwaambia waandishi hao kwamba kulikwa na kisa ambapo mtu mmoja alipigwa risasi na maafisa wa usalama nje kidogo ya ikulu. Alisema mtu aliyejeruhiwa alikuwa hospitalini, na kuongeza kwamba hali ilikuwa imedhibitiwa.

Baadaye, maafisa wa kulinda usalama wa rais walituma ujumbe kupitia mtandao wa Twtter na kuthibitisha kwamba afisa mmoja alimpiga risasi mtu mmoja karibu na White House.

MZEE MWENYE UWEZO WA AJABU KUTENGENEZA BUNDUKI, AWASHANGAZA RC NA DC “NIPENI FURSA

Soma na hizi

Tupia Comments