Donald Trump amesisitiza mpango wake wa kuidhibiti Gaza akisema amejitolea kununua na kumiliki ardhi hiyo iliyoharibiwa na vita lakini anaweza kuruhusu sehemu zake kujengwa upya na mataifa mengine ya Mashariki ya Kati.
Akizungumza kwenye ndege ya Air Force One akielekea kuhudhuria Super Bowl huko New Orleans, rais wa Marekani aliwaambia waandishi wa habari: “Nimejitolea kununua na kumiliki Gaza.
“Kuhusu sisi kuijenga upya, tunaweza kuipa mataifa mengine katika Mashariki ya Kati kujenga sehemu zake, watu wengine wanaweza kufanya hivyo, kupitia mwamvuli wetu. Lakini tumejitolea kuimiliki, kuichukua, na kuhakikisha kuwa Hamas hairudi nyuma.”
Aliongeza: “Hakuna cha kurejea ndani. Mahali ni hapo ni eneo la ubomoaji. Sehemu iliyobaki itabomolewa. Kila kitu kimebomolewa.