Top Stories

Trump atangaza kuuza kitabu chenye picha zake za Urais USD 74

on

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anataka kutengeneza faida kabla ya christmas sio? ni baada ya kutangaza kuingiza sokoni kitabu chake kipya cha picha ambacho kitakuwa tayari kabla ya December katikati kikiuzwa $74.99 (Tsh. 172,445) lakini kwa wale wataotaka kikiwa na saini yake ni $229.99 (Tsh. 528,879) kwa nakala moja.

“Kila picha imechaguliwa na mimi na kila maelezo mafupi ni yangu, mengine kwa mwandiko wangu mwenyewe, safari yetu ya pamoja ni mkusanyiko wa picha nzuri zilizonaswa wakati wa mafanikio yetu katika Ikulu ya White House, zipo behind the scenes pia, ni kitabu ambacho kila Mzalendo lazima awe nacho”

Hapa nimkuwekea picha mbalimbali kutoka kwenye website yake ya 45books.com ambako oda na manunuzi yatafanyiko huko ambapo inasemekana ameipa jina la 45books kwakuwa alikua Rais wa 45 wa Marekani.

ULIPITWA? PIKIPIKI YA UMEME, UKICHAJI INAKUTOA DAR MPAKA BAGAMOYO, INAUZWA MILIONI 6+

Soma na hizi

Tupia Comments