Donald Trump na Vladimir Putin wanaweza kukutana mapema mwezi huu, ingawa mkutano wa ana kwa ana utachukua muda kujiandaa, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema, kulingana na mashirika ya habari ya Urusi.
Peskov alisema mazungumzo ya Marekani na Urusi yaliyofanyika Jumanne mjini Riyadh ni “hatua muhimu” kuelekea kufikia suluhu kuhusu vita.
Lakini alisema uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu duniani itabidi kwanza uhuishwe upya kabla ya kurejeshwa.
Kwa muktadha: Jana, Trump pia alisema huenda akakutana na Putin mwezi huu na akatupilia mbali wasiwasi wa Ukraine kuhusu kuachwa nje ya mazungumzo nchini Saudi Arabia kuhusu kumaliza vita vya Ukraine.
Mkutano wa mjini Riyadh uliashiria hatua nyingine muhimu ya utawala wa Trump kubadili sera ya Marekani kuhusu kuitenga Russia.
Mapema mwezi huu, rais wa Marekani pia alisema yeye na Putin walikubaliana kuanza mazungumzo ya kumaliza vita baada ya kuwa na simu na kiongozi wa Urusi.