Mix

Utafiti wa Twaweza kuhusu Utendaji na siasa Tanzania

on

Taasisi ya utafiti ya Twaweza ilifanya utafiti kuhusu Matarajio na Matokeo katika Vipaumbele, Utendaji na siasa Tanzania na leo June 15 2017 wameizindua ripoti ya utafiti huo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze amelezea namna walivyo fanya mchakato huo.

Aidan Eyakuze amesema kuwa katika ripoti hiyo Wananchi wametaja tatizo la upungufu wa chakula kuwa ni kubwa sana kuliko ilivyokuwa miaka iliyopita na kwa upande mwingine ameelezea kushuka kwa asilimia 25 ya kukubalika kwa utendaji wa Rais.

….>>>“Kwanza tulienda kuongea na wananchi wapatao 1805 na ieleweke kwamba tunawahoji watanzania kwa ujumla wao na tumegundua kwamba kipato kuwa duni na uhaba wa chakula watanzania wengi wanasema kwamba haya mambo mawili ndio makubwa kwao katika shida wanazokutana nazo.

“Jambo la tatu tume wauliza jinsi wanavyo mkubali Rais Magufuli na utafiti huu umebaini kwamba kukubalika kwake kumeshuka mpaka aslimia 71 na tafsiri ni kwamba kushuka huko kunaendana na vipaumbele vya wananchi kubadilika” – Aidan Eyakuze

UFAFANUZI: TFDA kuhusu mchele wa plastic (+Video)

Soma na hizi

Tupia Comments