Habari za Mastaa

Taylor Swift aivunja rekodi ya Marehemu Whitney Houston

on

Mwanadada Taylor Swift amevunja rekodi na kumpiku msanii mkongwe  Marehemu Whitney Houston katika tuzo za American Music Awards ‘AMAs’ zilizofanyika October 9,2018 akiwa ameshinda jumla ya tuzo 23.

Taylor Swift anatajwa kuwa msanii pekee wa kike kushinda tuzo nyingi huku marehemu Whitney Houston ndio alikuwa akishikilia rekodi hiyo kwa kuwa na jumla ya tuzo 22 za AMAs

Taylor Swift ameondoka na jumla ya tuzo 4 akiwa ameshinda tuzo katika kipengele cha msanii bora wa Pop wa kike, Best Tour, Album bora ya muziki wa Pop ‘Reputation’ na tuzo kubwa ya msanii bora wa mwaka huku akiwatupa mbali Imagine Dragons, Drake, Ed Sheeran na Post Malone.

“Rafiki zangu nimewahi kuwasimulia mkasa wa Mbudya” -Haji Manara

Soma na hizi

Tupia Comments