Top Stories

“Tujipange, tutangaze shughuli za maadhimisho ya Uhuru” Waziri Kijaji

on

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Ashantu Kijaji amevitaka vyombo vya Habari nchini kuanza maandalizi ya kutangaza shughuli zote za maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru yaliyopangwa kufanyika Disemba 9 Mwaka huu.

Tanzania imeadhimisha sherehe za Uhuru mara ya mwisho mwaka 2019. Hata hivyo Serikali imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali hususani katika maeneo ya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar kuanzia November 2.

Dk. Kijaji amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama atakutana na vyombo vya Habari kutoa ratiba ya maadhimisho hayo.

“Naomba tujipange tutangaze shughuli za maadhimisho haya,” amesema nakutaka vyombo vya Habari kuteua waandishi waandamizi na makini kufanikisha shughuli za kuhabarisha umma kuhusu maadhimisho ya sherehe hizo.

MO DEWJI AKASIRIKA “HAIKUBALIKI, WALIOSABABISHA WACHUKULIWE HATUA”

Soma na hizi

Tupia Comments