AyoTV

VIDEO: Alichokiongea Naibu spika Dk. Tulia kuhusu walemavu wa macho nchini

on

Ikiwa leo October 6 2016 ni siku ya maadhimisho ya watu wenye ulemavu wa kuona walemavu wasioona ambapo kitaifa imefanyika mkoani Mbeya huku mgeni rasmi akiwa ni naibu spika Dk. Tulia Ackson, Serikali imetoa mikakati yake ikiwemo kuwawezesha walemavu kupata huduma za afya bure kupitia vitambulisho vya bima.

Akiongea na waannchi wa mkoa huo Dk. Tulia Ackson amesema….>>>’Serikali inamikakati ya kuwawezesha kiuchumi wananchi hususani watu wenye ulemavu ili kuboresha miradi yao ya kujikwamua kiuchumi

Kwa upande wa matibabu serikali imekamilisha utaratibu wa bima ya afya kwa wote wakiwemo wale wasioona bila kujali hali yake ya kipato, natoa wito kwa wakurugenzi wote wilaya hadi majiji kuwahamasisha wananchi kujiunga katika bima hizo na wale wasio na uwezo wagharamiwe na mamlaka husika‘ –Dk. Tulia

Unaweza kumsikiliza Naibu spika Dk. Tulia kwenye hii video hapa chini…

ULIIKOSA HII YA MAAMUZI YA SERIKALI BAADA YA KUIONA ILE VIDEO WALIMU WAKIMPIGA MWANAFUNZI

Soma na hizi

Tupia Comments