AyoTV

VIDEO: Naibu spika Dk. Tulia katangaza kuiendeleza jadi

on

Najua kuna watu wangu wana love ya kutosha pale wanaposikia suala la burudani, yes..! kama na wewe ni mmoja wapo basi hii si yakukosa, Naibu spika Dk. Tulia Ackson ametuandalia tamasha la ngoma za jadi litakalofanyika Tukuyu mkoani Mbeya kuanzia tarehe 7 hadi 8 mwezi October 2016.

Dk. Tulia amesema…>>>’Nimeandaa tamasha la ngoma za jadi litakalofanyika Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kuanzia October 7 hadi 8 2016 huku likiwahusisha wananchi mbalimbali wakiwemo wakazi wa Mbeya

Wazo hili nilikuwa nalo zamani lakini sasa nimepata fursa ya kufanya hivyo huku lengo likiwa ni kuzifanya ngoma za jadi zijulikane kwamaana zimekosa umuhimu kutokana na watu wengi wa vijijini kukimbilia mijini huku wakisahau tamaduni zao‘ –Dk. Tulia Ackson

Kwa washiriki waone hiyo kama moja ya fursa za kiuchumi kwakuwa hadi sasa nimetafuta wafadhili ili baadhi ya vijana wakapate nafasi ya kujiendeleza kimasomo katika chuo cha Bagamoyo, nataraji watu wa Rungwe na Kyela watajionea tamaduni zetu mbalimbali‘ –Dk. Tulia Ackson

Hizi ni tamaduni za Kinyakyusa ambazo nimepanga kuanza nazo lakini baadae tukijaaliwa tutaenda katika tamaduni za makabila mengine ikiwemo nchi nzima, katika tamasha kama hili lengo kubwa ni kukuza utamaduni kwamaana hiyo kila mtu ataingia na kushiriki bure‘ –Dk. Tulia Ackson

Unaweza kuyapata yote kwenye hii video hapa chini Dk. Tulia Ackson Akielezea…

ULIKOSA HII YA WABUNGE  WATORO KUPIGWA STOP KULIPWA POSHO 

Soma na hizi

Tupia Comments