Top Stories

Tulia apitishwa kugombea Uspika

on

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, imepitisha jina pekee la Dk. Tulia Akson kuwa mgombea wa kiti cha Spika kilichoachwa wazi na Job Ndugai aliyejiuluzu nafasi hiyo Januari 6, 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 20, 2022 kwenye ukumbi wa White House Dodoma, Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati Kuu imepitisha jina moja la Dk Akson kati ya majina 70 ya makada wa CCM waliochukua na kurejesha fomu.

Soma na hizi

Tupia Comments