Top Stories

Tume ya Mawasiliano Uganda yavionya vyombo vya habari

on

Baada ya kuripoti maandamano, Tume ya Mawasiliano nchini Uganda (UCC) imevitaka Vyombo vya Habari kuzingatia Kanuni na Taratibu hususan vinaporusha matukio mubashara.

Imesema, taarifa na matukio yanarushwa kwa namna ambayo inaweza kupotosha Umma huku ikitahadharisha kuhusu maudhui yanayoweza kuhatarisha Usalama wa Taifa.

Wanahabari wameelekezwa kutochapisha picha zenye maudhui ya kutisha ikiwemo vifo na majeruhi bila kutoa tahadhari kwa watazamaji.

Vyombo vya Habari vimekumbushwa kuzingatia Kanuni huku Mamlaka ikisema itawachukulia hatua wale watakaokiuka taratibu.

MATESO MAKALI ANAYOPATA MFUASI WA BOBI WINE, SABA WAMEUAWA

Soma na hizi

Tupia Comments