“Leo tunafikia mwisho wa maombolezo ya kitaifa yaliyotangazwa na Rais wa Nchi Mama Samia Suluhu Hassan siku ya tarehe 17 March kutokana na kifo cha shujaa wetu mwendazake JPM” DC Sabaya
“Kesho bendera zitarudi kwenye kimo chake shujaa JPM tumekuomboleza kwa siku 21, lakini nafsi zetu zitakusherehekea kwa kazi ulizofanya hadi tutakapokutana baadae!, kwa kuwa ni lazima tuamke sasa na kuishi urithi uliotuachia, tunakung’uta mavumbi rasmi na tunakoma kulia ili tusiwaumize wanaotegemea huduma zetu” DC Sabaya
“Tunaamka tena kwa faraja na hamasa ya mrithi wako anayeongoza vita kwa kutusalimu katika jina la”Jamhuri hii ya Muungano wa Tanzania, akitaka kazi iendelee” DC Sabaya
“AMESEMA” Acha dhoruba ipige, upepo uwe mwingi ila Lazima Jahazi lifike “. Endelea kupumzika kwa Amani, Huku duniani tutaendelea na kazi hadi tutakapokutana baadae kwenye pumziko la Milele” DC Sabaya ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram