Michezo

Patrice Evra ametangaza kutundika daruga, mtarajie kwa hili

on

Beki wa zamani wa club ya club za Man United na Juventus Patrice Evra leo July 29 2019 ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka, Evra amefikia maamuzi akiwa na umri wa miaka 38.

Evra ametangaza kustaafu soka na kunukuliwa akisema kuwa atakuwa tayari kuiongoza timu kwa maana ya kuwa kocha ndani ya miaka miwili ijayo, akiwa amecheza vilabu mbalimbali ikiwemo AS Monaco ya kwao Ufaransa Evra amecheza jumla ya michezo 700.

Mafanikio yake makubwa katika soka ni pamoja na kutwaa mataji matano ya Ligi Kuu ya England EPL, Ligi Kuu Italia mawili na taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kuichezea timu yake ya taifa ya Ufaransa jumla ya michezo 81.

Soma na hizi

Tupia Comments