Wakati diplomasia ikishika kasi na kwamba sauti za kupinga uingiliaji kati wowote wa kijeshi wa ECOWAS nchini Niger zimesikika baada ya mkutano wa wakuu wa majeshi, jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi halijatupili mbali hata kidogo chaguo la kuingilia kati kijeshi kurejesha demokrasia nchini Niger na rais Mohammed Bazoum kweye nafasi yake.
Kulingana na vyanzo vya karibu, mchakato unaendelea na mipango hiyo, ambayo iliidhinishwa mjini Accra na kwa sasa inatoa nafasi ya kutumwa kwa wanajeshi, inaendelea.
Viongozi wa kijeshi wa kikosi cha dharura wako tayari kutuma vikosi vyao nchini Niger, huku wakisema, “hatujapokea amri ya kupinga” kuingilia kijeshi nchini Niamey, kulingana na afisa mkuu. Kwa kwelii, chaguo la kuingilia kijeshi kurejesha utawala wa kikatiba nchini Niger bado ni muhimu, liko na linapangwa, anaripoti mwandishi wetu huko Cotonou, Jean-Luc Aplogan.
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, wakuu wa majeshi kwa sasa wanasimamia zoezi la kupelekwa kwa wanajeshi hao. Katika awamu hii ya uanzishwaji, nchi zilizo mbali na Niger zimekubali kutuma wanajeshi wao katika nchi zinazopakana na Niger, zilizochaguliwa kama ngome.
Hatua hii iko karibu, kulingana na duru za kuaminika: wanajeshi na vifaa wanaweza kusafirishwa kwa njia ya anga au baharini.
Taarifa za hivi punde zinaonyesha kuwa kikosi cha dharura cha ECOWAS kitaundwa na wanajeshi kutoka Benin, Nigeria, Senegal, Côte d’Ivoire, Guinea-Bissau, na sasa unazungumziwa mchango wa Ghana.
Ili kuashiria kujitolea kwake, Ghana iliandaa mkutano wa Wakuu wa Majeshi mnamo Agosti 18 na rais wake Nana Akoufo Ado aliwapokea maafisa wakuu waliohudhuria kwa takriban dakika arobaini.