Habari za Mastaa

“Tutafunga 02 Arena” P-square

on

Nyota wa muziki nchini Nigeria ambaye anaunda kundi la P-Square, Peter Okoye, ameweka wazi kuwa kundi hilo linao uwezo wa kufanya matamasha bila kutoa kazi mpya na yakafanya vizuri.

Hayo yanajiri baada ya wakali hao kuwataka mashabiki wao waliopo nchini Uingereza, kuchagua ni mahali gani wakafanye shoo kubwa kati ya Uwanja wa O2 Arena au Uwanja wa Taifa wa Uingereza wa Wembley.

Maoni ya mashabiki wengi yameuchagua 02 Arena unaoingiza takribani watu elfu 20.

Chaguo hilo ni kutokana na mfululizo wa wasanii nchini Nigeria kufanya show zao katika uwanja huo wakiwemo Wiz Kid, Davido, Burna Boy na wengineo ambapo mashabiki wametaka wakongwe hao nao wakaoneshe uwezo wao katika uwanja huo.

“Hatuhitaji kuujaza O2 Arena, tunaenda kuufunga kabisa, iwe tumeachia kazi mpya ama hatuna kazi mpya.

Mkongwe ni mkongwe,” amesema Peter Okoye akiwajibu mashabiki ambao wana wasiwasi kama kundi hilo linaweza kuujaza ukumbi huo.

Soma na hizi

Tupia Comments