Top Stories

“Tutashirikiana na Wapinzani” Rais Samia

on

“Tutakwenda kupata maendeleo ya haraka kwa sababu vyama viko vingi, macho yako mengi, miono iko mingi… maono yako mengi. Wanavyoona chama kimoja kiko ndani ya serikali pengine hawatakuwa na macho makubwa ya kuona kama wengine walio nje ya serikali” Rais Samia

“Ndio maana tukasema vyama vingi hivi, kazi yake ni kuangalia yanayoendelea, yanayoendeshwa na serikali na kutuoa maoni yao. Kwamba mbona tunakojipanga mpango wetu huu tunaoita dira ya Tanzania ingekwenda hivi… hiyo ndiyo kazi yetu” Rais Samia

“Kwa serikali kazi yetu ni kuwashirikisha katika hayo. Na mimi nataka nitoe ahadi kwenu kwamba tutashirikishana katika hayo kwa sababu Tanzania hii haitajengwa na mtu mmoja, haitajengwa na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu, iwe sera, sheria au dira lazima tujadili wote kama watanzania na tukikubaliana tunakwenda kutekeleza wote kama watanzania atakaye kiuka hapo ni mkosi” Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma leo.

Soma na hizi

Tupia Comments