Kufuatia wito wa Rais Samia Suluhu Hassan kutaka Wakandarasi wa ndani wanaopewa miradi mikubwa ya Serikali kuifanya kwa ufanisi mkubwa, Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Consulting Limited, Patrick Kasera kwa niaba ya wakandarasi wa ndani amemwakikishia Rais kuwa watafanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika miradi wanayopewa kuitekeleza.
Injinia Kasera amesema kampuni za ndani zinafarijika sana kwa hatua ya Serikali kuamua kutumia kampuni za ndani katika kutekeleza mradi mkubwa wa mashamba wenye lengo la kuwawezesha vijana kumiliki ardhi na kukifanya kilimo kuwa biashara.
Jana Rais Samia Suluhu jijini Dodoma alizindua mradi huo wa mashamba makubwa maarufu kama BBT ambapo ukimalizika utanufaisha vijana zaidi ya milioni tatu na kuondoa kabisa ukosefu wa chakula nchini.
“Kampuni yetu imepewa miradi mitano ya kujenga miundombinu wa ya umwagiliaji, tunamwakikishia Rais kwamba tunayafanyia kazi maagizo yake kwa vitendo kwa kuwa tuna vifaa vya kisasa na wataalam makini,’ alisema Kasera.