Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi amesema serikali imejipanga kuandaa mazingira bora ya uchaguzi kwa vyama vyote vya siasa nchini kuwa dhamira ya serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassani ni kuhakikisha chaguzi zote zitakazofanyika nchini kuwa zinazingatia misingi ya demokrasia.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anafanya ziara kwenye vyama vya siasa kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa kuiongoza wizara hiyo.
“Nataka niwatoe hofu vyama vyote 19 kuwa kwenye uchaguzi ujao chini ya Rais Samia utakuwa huru na wa haki,” amesema Lukuvi.
Waziri Lukuvi amevitaka vyama vyote vitakavyoshiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kujiandaa kushindana kwa sera ili wananchi waamue.
Aidha , Waziri Lukuvi amesema lengo la ziara hiyo ni ya kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa nafasi hiyo.
Amesema katika wizara yake anasimamia (Sera, Bunge na Uratibu) moja ya majukumu ni kuvisimamia vyama vya siasa hivyo atavitembelea vyama vyote 19.
Katika ziara hiyo waziri lukuvi aliambatana na Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wamesema ziara hiyo itaongeza hamasa ya ushirikiano
Mwenyekiti wa chama cha CHAUMA Hashim rungwe amempongeza Waziri Lukuvi kwa kufanya ziara hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.