Michezo

Mechi iliyochezwa bila mashabiki, bila goli bila konyeshwa kwenye TV

on

Korea Kusini na Korea Kaskazini jana zilitoka sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa kihistoria na wa ajabu wa kufuzu Kombe la Dunia, uliochezwa mbele ya uwanja uliokuwa mtupu na kufungwa kwa ulimwengu wa nje.

Mchezo kati ya pande mbili ambazo nchi zao kimsingi zipo vitani, ulifanyika katika uwanja wa Kim Il Sung mjini Pyongyang bila kutangazwa moja kwa moja, ama kuwepo mashabiki na hata vyombo vya habari vya nje pia havikuruhusiwa.

Nyota wa Tottenham Hotspur Son Heung-min alibeba unahodha wa Korea Kusini kwenye mechi ya kwanza yenye ushindani iliyochezwa Pyongyang huku mashabiki wa Korea Kusini ambao wamejawa na hasira, kwa kutoruhusiwa kwenda kungalia mechi, watalazimika kusubiri kwa siku nyingi kuona mechi hiyo kwenye televisheni, baada ya maofisa kupeleka DVD iliyorikodiwa mchezo huo.

HARMONIZE AMKOSHA MAGUFULI ATAKA KUMPA UBUNGE, AMTAJIA JIMBO

Soma na hizi

Tupia Comments